Monday, 17 November 2014

Mbeya City yajiondoa ubingwa wa Ligi Bara



hare
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe,  alisema kwa sasa hawana ndoto za kutwaa ubingwa ama kumaliza kwenye nafasi za juu kama msimu uliopita, hivyo wanajipanga kuhakikisha timu inabaki Ligi Kuu na ndipo mipango mingine iendelee.

TIMU ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imetangaza kujiondoa rasmi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuanza vibaya kwenye mechi saba na akili zote sasa wamezielekeza katika kuiokoa timu hiyo na janga la kushuka daraja.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe,  alisema kwa sasa hawana ndoto za kutwaa ubingwa ama kumaliza kwenye nafasi za juu kama msimu uliopita, hivyo wanajipanga kuhakikisha timu inabaki Ligi Kuu na ndipo mipango mingine iendelee.
Mbeya City ilifanya vizuri msimu uliopita na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu lakini imeanza vibaya msimu huu baada ya kushinda mchezo mmoja pekee kati ya saba huku ikiwa imefungwa mechi nne na kuishia kushika mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano.
“Tumejiondoka rasmi kwenye mbio za ubingwa, kwa sasa tumeweka akili zote katika kuhakikisha timu inasalia Ligi Kuu kwani ikishuka daraja itakuwa ni majanga,” alisema.
“Kuhusu taarifa za kocha Juma Mwambusi kujiuzulu bado hatujapokea barua rasmi, jana (Juzi Jumamosi) haikuwa siku ya kazi, leo pia (Jana Jumapili) siyo siku ya kazi, nadhani kesho (leo Jumatatu) tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia.
“Kama kajiuzulu kweli tutafanya utaratibu wa kupata kocha mwingine.”

No comments:

Post a Comment