Traore atawasili nchini baada ya kumaliza mechi yake ya Jumatano ijayo ambayo atakuwa akiichezea timu yake ya Taifa ya Mali itakayocheza na Algeria kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na atakuwa mchezaji wa pili kutoka El Merreikh baada ya Muivory Coast Pascal Wawa aliyepewa mkataba wa miaka miwili.
MATAJIRI Azam FC wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumnasa straika Mmali wa El Merreikh, Mohamed Traore ambaye anatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa mwezi huu kwa mazungumzo ya mwisho, pia klabu hiyo imetangaza dau analouzwa Muivory Coast wao, Kipre Tchetche ni Sh336 milioni.
Traore atawasili nchini baada ya kumaliza mechi
yake ya Jumatano ijayo ambayo atakuwa akiichezea timu yake ya Taifa ya
Mali itakayocheza na Algeria kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika na atakuwa mchezaji wa pili kutoka El Merreikh baada ya
Muivory Coast Pascal Wawa aliyepewa mkataba wa miaka miwili.
Azam inamsajili Traore ambaye atakuwa mchezaji wa
tano wa kigeni baada ya Tchetche, Wawa, Muivory Coast Kipre Bolou,
Mrundi Didier Kavumbagu na Mhaiti Leonel Saint-Preux baada ya kumtupia
virago Mmali, Ismail Diara.
Na ili kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa
kigeni wanaohitajika Ligi Kuu Bara, inaweza kumuuza Tchetche ambaye
anatakiwa na klabu mbalimbali kutoka Malaysia na Sri- Lanka kwa
makubaliano ya kulipwa kiasi hicho cha pesa au Leonel.
Akimzungumzia Tchetche kigogo mmoja wa Azam
alisema: “Kuhusu Tchetche yuko sokoni lakini wanaomhitaji wafahamu dau
lake ni Dola 200,000.”
Katika hatua nyingine, Azam itaanza maandalizi
yake leo Jumatatu na wachezaji wote wataanza mazoezi Uwanja wa Chamazi
isipokuwa wale waliokuwa na timu zao za Taifa.
Mmoja wa maafisa wa El Merreikh ameliambia
Mwanaspoti kuwa, klabu yake ilikubaliana na Wawa kuvunja mkataba wake
uliobakiza miaka miwili na aondoke kama mchezaji huru kwani mwenyewe
aliomba kuondoka.
“Wawa tulikubaliana naye aondoke baada ya kutuomba
kwani amecheza kwetu kwa miaka mitano na kuitumikia klabu asilimia 96,
sasa mtu mliyeishi naye vizuri akiomba kitu lazima mumsikilize hivyo
ameondoka kama mchezaji huru.
“Lakini katika kuondoka kwake ametuachia kasheshe
hapa kwani mashabiki wamekasirika, hawaelewi kilichotokea lakini
hatukuwa na jinsi kwani Wawa alituambia hata kama akibaki hana uhakika
na uwezo wake utakavyokuwa,” alisema kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment