Jaguar ajitolea kutumbuiza watoto
Jaguar,
msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, ameendelea kuonyesha moyo wake wa
upendo kwa jamii, safari hii akiwa amejitolea muda wake kukutana na
watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na kufurahia wakati mzuri
pamoja nao.

Msanii Jaguar akiwa na watoto jukwaani
Jaguar
ametumia nafasi hii kutoa burudani kwa kuimba mbele ya watoto hawa kwa
lengo la kuwaburudisha kwa moyo wote katika jukwaa licha ya hali yao ya
matatizo ya akili.
Tukio hili linaongeza alama katika rekodi ya matukio ya msanii huyu kurudisha shukrani kwa jamii kwa misaada ya aina mbalimbali kuanzia kusaidia vituo mbalimbali vya watoto yatima mpaka kusomesha watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

No comments:
Post a Comment