
Anakwambia ‘tukiwa angani Rubani ambae ni rafiki yangu alijisikia vibaya ghafla na kuzimia kutokana na mshtuko wa moyo hivyo nikafikiria kuwa lazima nichukue usukani niendeshe lakini sikuwa nafahamu ninachopaswa kufanya hivyo nikaita radio call ili nipate msaada’ – John

‘Helicopter ilinifata kutoa msaada wa jinsi ya mimi kutua nikawa nafata maelekezo yao kiukweli nilikua sijui nibonyeze nini na nilipojaribu kutua sikuweza kuona barabara ya kutua hivyo ilishindikana japo baadae baada ya majaribio kadhaa iliwezekana kutua, nilitua kwanza na tairi la mbele lakini cha kusikitisha rubani alikua amefariki, familia yake iliomba jina la Marehemu lisitajwe popote hata na Polisi’
No comments:
Post a Comment