Thursday, 7 January 2016

HOTUBA YA KWANZA YA ZIDANE KWA REAL MADRID

Kocha mpya wa Real Madrid Zinedine Zidane
 Kocha mkuu wa mpya wa Real Madrid ambae aliwahi kuichezea clab hiyo
Zinedine Zidane, amewataka Wachezaji wake kuwa na nia moja kwa kila mchezaji kufanya kazi kwa bidii.

Wachezaji wengi wa timu hiyo wameshukuru kuondolewa kwa Rafa Benitez ambapo wamepata morali mpya baada ya kuteuliwa kwa Zinedine Zidane kuwa wanaheshimu ujio wake.
Wachezaji hao wa Real Madrid wakiongozwa na mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo, wameapa kuwa na utiifu kwa kocha huyo na wameahidi kufanya kazi kwa bidii na umoja wa kitimu katika clab hiyo.
Kabla ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, Zidane aliwahutubia wachezaji wote na kuwaelezea mwongozo wake wenye msisitizo wa mambo mawili makuu ambayo ni kazi kwa bidii na kufurahia kazi hiyo.
Katika kuimarisha kikosi cha kwanza cha Real Madrid, Zidane, amewachukua wachezaji watatu kutoka kikosi B, ambacho hujulikana kama Castilla ambao ni Borja Mayoral na viungo Marcos Llorente na Martin Ødegaard ili waanze kufanya mazoezi katika kikosi cha kwanza.
Wakati huo huo imeripotiwa kuwa Real Madrid inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 100 kwa ajili ya kuwania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard katika majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment