Monday, 1 September 2014

LUIS SUAREZ AREJEA LIVERPOOL LEO

  LUIS SUAREZ AREJEA LIVERPOOL LEO KUKUANYA VIRAGO VYAKE NA KUMKABIDHI STEVEN GERRARD UZI WA BARCA

MSHAMBULIAJI Luis Suarez amerejea kwenye viwanja vya mazoezi vya Liverpool katika siku ya leo ya mwisho ya usajili... lakini nyota huyo aliyehamia Barcelona kwa Pauni Milioni 75 alikwenda kuchukua mizigo yake tu.
Marafiki wameungana tena: Luis Suarez akiwa na Steven Gerrard (na jezi ya Barcelona) viwanja vya Melwood leo
 Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwasili akiwa na zawadi ndogo kwa Steven Gerrard - jezi ya Barca yenye nina lake- na Nahodha huyo wa Liverpool ameposti picha hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram.
Iliambatanishwa na ujumbe usemao: "Amekuja na zawadi kusema kwaheri kwa mtu muhimu asubuhi hii, namtakia mafanikio makubwa mchezaji,". 


Marafiki wameungana tena: Luis Suarez akiwa na Steven Gerrard (na jezi ya Barcelona) viwanja vya Melwood leo

No comments:

Post a Comment