MKONGWE
Ryan Giggs alimtamanisha kocha wake Louis van Gaal baada ya kufunga bao
moja magwiji wa Manchester wakifungwa 5-1 na Salford City, timu ambayo
kwa sasa anaimiliki kwa pamoja na Paul Scholes, Nicky Butt na Gary na
Phil Neville katika mchezo wa hisani uliovutia mashabiki 12,000 Uwanja
wa AJ Bell mjini Eccles.
Nyota
hao waitwao ‘Class of 92’ pamoja na kuonyesha ufundi bado upo, lakini
walizidiwa nguvu na kasi na vijana wadogo wa timu ya Daraja la Kwanza
kaskazini. Rio Ferdinand alisafiri kutoka kwenda kuwa kocha Msaidizi, lakini hakuinusuru timu yake ya zamani na kichapo.

No comments:
Post a Comment