Tuesday, 19 August 2014
SUAREZ AANZA KAZI RASMI BARCELONA IKIUA 6-0 NA KUTWAA KOMBE
MSHAMBULIAJI
Luis Suarez jana ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya,
Barcelona ikishinda mabao 6-0 Uwanja wa Camp Nou dhidi ya FC Leon, baada ya kupunguziwa adhabu na CAS.
Suarez
alifungiwa kujihusisha kabisa na soka kwa miezi minne baada ya
kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italia kwenye Kombe la Dunia, lakini CAS
inapunguza makali yake ya soka kwa kumruhusu kufanya mazoezi na kucheza
mechi zisizo za mashindano za Uruguay na Barcelona.
Na jana akaingia kuchukua nafasi ya Rafinha dakika ya 76, wakati huo tayari Barca inaongoza 4-0.
Friday, 8 August 2014
GIGSS AIFUNGIA MAN UNITED IKICHAPWA 5-1 NA KITIMU CHA DARAJA LA KWANZA
GIGSS AIFUNGIA MAN UNITED YA WAKONGWE IKICHAPWA 5-1 NA KITIMU CHA DARAJA LA KWANZA
MKONGWE
Ryan Giggs alimtamanisha kocha wake Louis van Gaal baada ya kufunga bao
moja magwiji wa Manchester wakifungwa 5-1 na Salford City, timu ambayo
kwa sasa anaimiliki kwa pamoja na Paul Scholes, Nicky Butt na Gary na
Phil Neville katika mchezo wa hisani uliovutia mashabiki 12,000 Uwanja
wa AJ Bell mjini Eccles.
Nyota
hao waitwao ‘Class of 92’ pamoja na kuonyesha ufundi bado upo, lakini
walizidiwa nguvu na kasi na vijana wadogo wa timu ya Daraja la Kwanza
kaskazini. Rio Ferdinand alisafiri kutoka kwenda kuwa kocha Msaidizi, lakini hakuinusuru timu yake ya zamani na kichapo.
Pichaz za baadhi ya Wasanii waliotua Mwanza tayari kwa ajili ya Serengeti fiesta kesho CCM Kirumba
Wasanii hao ni wale ambao wataperfoam kesho waliofika ni pamoja na Ney wa Mitego,Young D,Mr.blue,Barakah Da Prince,Chegge na Temba,Madee,Makomando,Stamina,Young Killer,Vanessa Mdee na wengine kibao.
Miongoni mwa wasemaji wa mkutano huu na waandishi wa habari ni pamoja na Mwenyekiti wa shamrashamara za Serengeti Fiesta Sebastian Maganga ambaye amesema kuwa sababu ya kuanza kwa Serengeti Fiesta kwa mkoa wa mwanza ni kama watu wana kumbukumbu mwaka 2004 Serengeti Fiesta ya kwanza kutoka nje ya Dar ilikua ni ndani ya jiji la Dar ambayo ilikua na kauli mbiu ya Utamaduni unaendelea.
Kwa miaka 10 hii kwa sasa wameweza kushuhudia namna ilivyosambaza upendo ambayo imewajumuisha wasanii wadogo na wakubwa na safari hii Serengeti fiesta imeongeza miji na itakuwa miji 18 badala ya 14 ya mwaka jana.
Hizi ni baadhi ya picha za mkutano huo.

JACK WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA NAY!
Subscribe to:
Comments (Atom)

