
Algeria ilifanikiwa kuingiza bao moja la kufuta machozi dhidi ya Ujerumani
Timu mbili za mwisho za Afrika
katika kombe la dunia zimendoka dimbani baada ya kushindwa katika awamu
ya timu bora kumi na sita.
Nigeria walicharazwa na Ufaransa mbili bila huku Algeria ikiangushwa na Ujerumani mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada.Algeria na Nigeria walijitahidi kadri ya uwezo wao kuingia katika awamu ya robo fainali ingawa mambo yalikuwa magumu.

Nigeria ilichapwa mabapo mawili bila na Ufaransa
Katika muda wa ziada walichapwa mabo mawili ingawa walifanikiwa kuingiza bao moja kabla ya muda kumalizika. Matumaini ya kusonga mbele yakaisha.
Katika mechi yao, mabingwa wa Afrika, Nigeria walikula kichapo cha mabao mawili bila dhidi ya Ufaransa na baada ya mechi kumalizika, kocha wa timu yao Stephen Keshi akajiuzulu.
No comments:
Post a Comment