KLABU
ya Arsenal imesajili kinda la thamani ya juu kutoka timu ya vijana ya
Barcelona, Georgios Spanoudakis, ambaye awali nalikataa ofa kibao za
timu ya Arsene Wenger.
Kinda
hilo la miaka 15 linalocheza nafasi ya kiungo cha kati lilijiunga na
akademi ya Katalunya, La Masia likitokea Eintracht Frankfurt mwaka 2009,
lakimi sasa linajiunga kikosi cha Arsenal cha vijana chini ya umri wa
miaka 18 kuanzia msimu ujao.
Spanoudakis
amechezea mechi kadhaa timu za taifa za vijana za Ujerumani, lakini
bado anaweza kuamua kucheze Ugiriki akitaka kubadilisha uraia.

No comments:
Post a Comment