![]() |
Andrew Chenge |
Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato.
Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.
“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.
“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge.
Alisema wakati Serikali ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato, Deni la Taifa lililofika Sh30 trilioni sawa na asilimia 57 ya pato la taifa ni mzigo wa taifa na tishio kwa utengamavu wa uchumi jumla.
“Uwiano uliopo wa Deni la Taifa na Pato la Taifa kiuchumi siyo wa kuridhisha. Ukubwa wa deni hili hauwiani na kiwango cha uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa sasa wa asilimia 7.0,” alisema na kuongeza:
“Yalifanyika manunuzi ya Dola za Marekani 810,000 katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambayo hayakupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali.”
Alisema tatizo la kutokusimamia kwa umakini matumizi ya Serikali lilisababisha Bajeti ya mwaka 2013/14 kuanza na deni Sh611.4 bilioni, ambazo ni matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na kwamba deni hilo halikuingizwa kwenye bajeti ya 2013/14… “Hali hii inatarajiwa pia kujitokeza tena kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye bajeti ya mwaka 2014/15. Malimbikizo ya madai hayo hadi Desemba 2013, yalifikia Sh2 trilioni sawa na asilimia nne ya pato la taifa. Tatizo hili ni lazima litafutiwe dawa haraka,” alisema Chenge.
Alisema ongezeko la Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15 kwa Sh1.605 trilioni, ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayomalizika ya mwaka 2013/14 linatia shaka iwapo malengo ya ukusanyaji na matumizi yatafanikiwa.
Alisema katika mwaka wa fedha 2013/14 utekelezaji wa bajeti katika baadhi ya mafungu ulifanyika kinyume na matarajio ya Serikali, kwa maelezo kuwa yapo baadhi ya mafungu ambayo hayakutengewa fedha lakini walipewa fedha nje ya bajeti za fungu husika.

a uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14, Chenge alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na vinywaji vikali, kumepitwa na wakati.
Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni.
Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.
“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.
“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge.
Alisema wakati Serikali ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato, Deni la Taifa lililofika Sh30 trilioni sawa na asilimia 57 ya pato la taifa ni mzigo wa taifa na tishio kwa utengamavu wa uchumi jumla.
“Uwiano uliopo wa Deni la Taifa na Pato la Taifa kiuchumi siyo wa kuridhisha. Ukubwa wa deni hili hauwiani na kiwango cha uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa sasa wa asilimia 7.0,” alisema na kuongeza:
“Yalifanyika manunuzi ya Dola za Marekani 810,000 katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambayo hayakupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali.”
Alisema tatizo la kutokusimamia kwa umakini matumizi ya Serikali lilisababisha Bajeti ya mwaka 2013/14 kuanza na deni Sh611.4 bilioni, ambazo ni matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na kwamba deni hilo halikuingizwa kwenye bajeti ya 2013/14… “Hali hii inatarajiwa pia kujitokeza tena kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye bajeti ya mwaka 2014/15. Malimbikizo ya madai hayo hadi Desemba 2013, yalifikia Sh2 trilioni sawa na asilimia nne ya pato la taifa. Tatizo hili ni lazima litafutiwe dawa haraka,” alisema Chenge.
Alisema ongezeko la Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15 kwa Sh1.605 trilioni, ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayomalizika ya mwaka 2013/14 linatia shaka iwapo malengo ya ukusanyaji na matumizi yatafanikiwa.
Alisema katika mwaka wa fedha 2013/14 utekelezaji wa bajeti katika baadhi ya mafungu ulifanyika kinyume na matarajio ya Serikali, kwa maelezo kuwa yapo baadhi ya mafungu ambayo hayakutengewa fedha lakini walipewa fedha nje ya bajeti za fungu husika.
Kambi hiyo ilipendekeza maeneo mapya ya ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta isiyo rasmi, wachimbaji wadogo wa madini na mapato ya kodi ya ardhi na maliasili.
Mengine ni mauzo ya mazao ya misitu, mapato ya uwindaji wa kitalii, mrabaha wa madini, taasisi za kibiashara za Serikali na mamlaka ya bandari.
Alipendekeza maeneo ya kipaumbele katika bajeti yao kuwa ni utawala bora, elimu, kilimo, afya, miundombinu, nyumba na makazi.
Mengine ni michezo na sanaa, ajira (kukuza uchumi vijijini) na ulinzi wa rasilimali za Taifa (wanyama, misitu, ardhi, uoto wa asili, maziwa, mito, bahari pamoja na mazao yake).
“Kambi Rasmi ya Bunge inapendekeza mishahara ya walimu iboreshwe na Serikali itoe misamaha ya kodi ya (Paye), kwenye mishahara ya walimu kama motisha ya kuwavutia wote wenye uwezo na sifa kufundisha, kuweza kufanya kazi zao kwa uadilifu.”
Akizungumzia kuhusiana na ukusanyaji wa mapato, Mbatia alisema kampuni za uwekezaji kwenye utafutaji na uchimbaji madini nchini zinapatiwa kivutio kadhaa kuendeleza shughuli zao nchini lakini kiasi kinachosamehewa kwa wawekezaji nchini huikosesha Serikali mapato ambayo ingeyapata kwa wawekezaji kwa kulipa kodi stahiki.
Nyingine ni msamaha wa mapato juu ya mtaji, wa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuagiza bidhaa ndani au nje ya nchi pamoja na kampuni na makandarasi wake.
Alisema baada ya kulipa kodi ya asilimia 0.3 kampuni hizo hulipa Dola 200,000 za Marekani tu kwa mwaka bila kujali ukubwa wa shughuli za uzalishaji, faida na uchafuzi wa mazingira na madhara mengine katika jamii.
Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa – NCCR – Mageuzi alisema kwa mujibu wa CAG, misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni za uchimbaji wa madini pekee kwa mwaka 2011, ilikuwa Sh109,885 bilioni huku misamaha iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ikifikia Sh239.667 bilioni.
No comments:
Post a Comment