Thursday, 27 February 2014

MZOZO WA GESI YA MTWARA WAHAMISHIWA TANGA


 


 


Mkuu wa mkoa wa Tanga Bi.Chiku Gallawa ametangaza kuwa utafutaji wa mafuta na gesi katika pwani ya mkoa huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu.\

Bi.Gallawa alisema kuwa shughuli hiyo ilipangwa kuanza mwezi mwezi uliopita lakini ilicheleweshwa ili kuwezesha
kampuni ya utafutaji kupata muda mrefu kujitayarisha.
Alisema kuwa utafutaji mafuta na gesi jambo kubwa ambalo linahitaji fedha nyingi,vifaa na utaalamu.


Hata hivyo alisema licha ya kuwa shughuli hiyo bado haijaanza,baadhi ya wenyeji wa wilaya za Mkinga na Tanga tayari wananufaika na kutokana na misaada mbalimbali inayotolewa na kampuni hiyo.
 Mkuu huyo mkoa alisema kampuni ya utafutaji imetenga shilingi milioni 300 kwa kila wilaya ambazo zitatumiwa katika miradi ya kijamii ikiwa ni pamoja na uchimbaji visima na ujenzi wa zahanati vijijini.

No comments:

Post a Comment