Tasnia ya bongo movies tumepata pigo baada ya mwigizaji mwenzetu Jaji Khamis (
kashi) alifariki dunia katika hospitali ya muhumbili alipokuwa amelazwa.
Msiba huu unakuwa ni mwendelezo wa majanga na misiba inayowakumba
wasanii na watu maafuru nchini ikiwa ni siku chache tuu zimepita toka
tulipomzika msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea aliyefariki
huko Afrika ya kusini
Tukiwa bado kwenye wiki hii ya msiba tumeweza kupata comments za mastaa
tofauti wa tasnia ya uigizaji waliyosema jana baada ya taarifa za msiba
wa kashi kuwafikia. Ila jambo ambalo limeonekana kuwatatiza wote jana
ni “kwanini maisha ya wasanii yanakatika hivi”? Why? Ni Swali gumu na
ambalo wengi wetu hatuwezi kuwa na jibu moja la uhakika maana Mungu ndo
ajuaye yote na muweza yote. Apangalo Maanani hamna anayeweza kulipangua.
Cha msingi ni kukaa katika njia zake yeye.hii ni kwamujibu wa blog ya The
Capital Tanzania
No comments:
Post a Comment